Ijumaa 30 Januari 2026 - 22:00
Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ni nembo ya kusimamia misingi thabiti mbele ya ubeberu wa kimataifa

Hawza/ Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Hasan Mousavi, katika tamko lake, amemuelezea Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kuwa ni mfano wa kivitendo wa uimara wa kiroho, kimaadili na kisiasa.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Hasan Mousavi, Rais wa Jumuiya ya Kisheria ya Mashia wa Jammu na Kashmir, katika tamko lake, amemtaja Ayatollah Mkuu Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, kuwa ni kielelezo wazi, kwenye mamlaka ya kiroho, kimaadili na kisiasa.

Aliendelea kusema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, licha ya mashinikizo makubwa ya kimataifa na kauli tata za hivi karibuni za Donald Trump, Rais wa Marekani, Iran imeendelea kusimama imara juu ya misingi yake, imani yake na uongozi wake wa kimaadili.

Mwanazuoni huyu mashuhuri wa Kashmir aliendelea kusema: Uongozi wa Iran, kwa mwanga wa maelekezo ya Mtukufu Imam Ruhullah Khomeini (rehema ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake) na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu Mtukufu Ayatollah Imam Khamenei (Mwenyezi Mungu aendeleze kivuli chake), haukusimama kwa kutegemea nguvu za kijeshi au kiuchumi pekee, bali umesimama juu ya misingi ya kimungu, haki, uadilifu na ujasiri wa kimaadili mbele ya mashinikizo ya kimataifa.

Akitolea mfano wa Qur’ani na kihistoria, alisisitiza: Firauni, kwa kutegemea jeshi, mali na nguvu, aliwadhulumu Wana wa Israil, lakini hatimaye kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu alizamishwa baharini (Surat Yunus, aya 90–92).

Vivyo hivyo, Nimrodi alikataa ujumbe wa Nabii Ibrahim (a.s) na akajenga utawala uliosimama juu ya dhulma na kiburi, lakini mwishowe alikumbana na kushindwa kwa aibu mbele ya haki na uadilifu.

Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Hasan Mousavi aliongeza: Mifano hii inaonesha wazi kwamba nguvu ya kweli haipo katika dhulma, utajiri au mashinikizo, bali imo katika misingi, imani na uimara wa kimaadili. Mtukufu Imam Khomeini (r.a) aliweka mantiki hii kama njia ya kusimama kwa uthabiti, heshima na hadhi mbele ya ubeberu wa kimataifa, na Mtukufu Ayatollah Imam Khamenei (Mwenyezi Mungu aendeleze kivuli chake) ameendeleza njia hiyo kwa msimamo wa kivitendo na wa kimaadili.

Aliendelea kusema kuwa; kauli za Trump ni dalili ya udhaifu wa ubeberu wa kimataifa na kuongezeka kwa nguvu ya muhimili wa muqawama wa Iran, na akabainisha: Taasisi za kimataifa zilizoanzishwa baada ya Vita ya Pili ya Dunia, leo zimekumbwa na udhaifu na kushindwa kwa wazi.

Rais wa Jumuiya ya Kisheria ya Mashia wa Jammu na Kashmir aliwataka Waislamu duniani, mataifa huru na serikali huru kulaani uvamizi na mienendo ya kibeberu ya Marekani, na kuunga mkono katika ngazi ya kimataifa msimamo wa kimsingi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Mwishoni huku akirejea aya ya Qur’ani Tukufu, alisema:
«إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُم لِيَصُدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّهِ فَسَيُنفِقُونَهَا ثُمَّ تَكُونُ عَلَيْهِمْ حَسْرَةً ثُمَّ يُغْلَبُونَ وَالَّذِينَ كَفَرُوا إِلَى جَهَنَّمَ يُحْشَرُونَ»

Hakika wale walio kufuru hutoa mali yao ili kuzuilia Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi watayatoa, kisha yatakuwa juu yao majuto, na kisha watashindwa. Na wale walio kufuru watakusanywa kwenye Jahannam.
(Surat Al-Anfal, aya ya 36)

Akasisitiza: Leo Iran si nchi tu, bali ni falsafa hai, nembo ya muqawama wa kimaadili, na taa ya uongofu wa kiroho na kisiasa kwenye ulimwengu wa Kiislamu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha